WILLIAM CHARLES

Naitwa William Charles Amani, nimezoeleka na wengi kwa jina la Charles William, ni mtangazaji wa kipindi cha East Africa Breakfast kinachosikika East Africa Radio, Jumatatu mpaka Ijumaa saa kumi na moja alfajiri mpaka saa tatu kamili asubuhi, pamoja na kipindi cha Weekend Breakfast kinachosikika Jumamosi saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa nne asubuhi.

 

Nimesoma na kuhitimu Shahada ya Sanaa katika Mawasiliano kwa Umma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nimekuwa katika tasnia ya habari na mawasiliano kwa umma tangu mwaka 2014, kama Mtangazaji wa televisheni, mwandishi wa habari za uchunguzi magazetini na Masscommunication practitioner katika taasisi mbalimbali kwa nyakati tofautitofauti. Nimebobea katika uchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii pamoja na uandishi wa habari za kuchunguzi.

 

Mimi pia ni mbobezi katika eneo la uandishi wa habari za kiuchambuzi na kiuchunguzi za usalama barabarani, zinazolenga kushawishi mabadiliko ya tabia, sera, sheria na uwajibikaji nikiwa nimehitimu mafunzo maalum ya miezi sita ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na Mfuko wa Wakfu wa Vyombo vya habari (TMF) mwaka 2017, yanayojulikana kama Bloomberg Initiative for Global Road Safety (BIGRS).
 

Ninaamini katika uchambuzi na uchunguzi kama njia ya kupata ukweli wa mambo katikati ya taarifa kinzani. Nje ya majukumu yangu ya kikazi, mimi ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu, mpenzi mkubwa wa kusikiliza muziki, kutazama mpira wa kikapu, na masumbwi. Ni mcheshi na ninayependa kujifunza mambo mapya kila siku, nikielewa kuwa kutoelimika ni gharama kuliko kujielimisha.