MWANNE OTHMAN

Mwanne Othman pia anajulikana kama Toto la Matashtit mwanadada mcheshi mwenye taaluma ya Uandishi wa Habari.Mtangazaji wa East Africa Radio kipindi cha Tam Tam Za Mwambao kinachoruka kila Jumapili kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 6 mchana.Mbali ya kipaji chake cha utangazaji pia ni 'bloger' na mwimbaji wa muziki wa taarab na mduara.Mmoja ya wimbo aliyoshirikishwa na mwanamziki mwingine ulishinda zawadi za Kilimanjaro mwaka 2011/2012.