MARYAM KITOSI

Naitwa Maryam David Kitosi, Nasikika kwenye Supamix kila Jumatatu mpaka
Ijumaa saa 3 asubuhi mpaka saa 6 mchana.

Kipaji cha utangazaji nilichonacho sikukigundua mapema mpaka nilipokuwa
kwenye harakati za maisha na kutafuta kazi nikajikuta nimeingia huko na
kuwa mmoja kati ya watangazaji bora Tanzania na anayependwa pia kwa
mujibu wa Tuzo za watu zilizofanyika mwaka 2014 na mwaka 2015 ambazo
nilikuwa nominated kama 'Mtangazaji wa Radio anayependwa' na kufanikiwa
kuingia fainali.

Napenda muziki, kusikiliza radio na kuangalia vipindi vya muziki,
lifestyle na kijamii kwenye televisheni ili kujifunza vitu na mbinu
mbalimbali kwenye kazi yangu na maisha kwa ujumla.

Kwangu utangazaji sio kazi tu bali ni kitu nafurahia kukifanya