JAY R JUNIOR

Unaweza ukamsikiliza Juma Masemo aka ‘Jay R Junior’ kila jumatatu hadi ijumaa kwenye Planet Bongo na jumamosi saa 4:00-6:00 mchana kwenye Bongo Fleva Top 20.
 
JR Junior aliingia kwenye kazi ya utangazaji kutokana na ndoto alizokua nazo tangu mdogo, alikua anapenda sana muziki,mpira pamoja na kufuatilia vipindi mbalimbali vya burudani kwenye Tv na Radio mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
 
JR amekua mfano kwa vijana wengi wa rika lake mtaani kwao kutokana na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kutumia vipaji walivyonavyo katika kujiendeleza kiuchumi.
Mbali na utangazaji Juma ni msanii wa kuimba, mchezaji mpira na mwandishi wa stori za filamu na maigizo.
 
Kwa moyo wa kuwasaidia vijana wenye vipaji Juma ameanzisha Bonanza la "Okoa sanaa" ambalo limeweza kuwakusanya pamoja vijana wengi jijini Tanga na kuonesha vipaji vyao.
 
Nimpenzi wa kukaa na watu wa rika lote ili kubadadilishana mawazo, kusafiri, kujifunza vitu vipya pamoja na kusaidia katika shughuli za kijamii ili kuchangia kuleta maendeleo.