GRAYSON GIDEON

Huyu ndiye mtayarishaji wa kipindi cha Planet Bongo ndani ya East Africa Radio kinachoruka kila siku za wiki jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 7 mchana hadi 10 jioni.
Pia ni mtangazaji wa kipindi cha Weekend Breakfast kila jumapili saa 12 asubuhi hadi saa 4 asubuhi.
Ndoto yake ya kuwa mtangazaji ilianza tangu akiwa shule ya sekondari lakini changamoto ikawa aina ya marafiki waliomzunguka ambao walikuwa wakiamini ni vigumu kufikia ndoto yake kwakuwa hakuwa na watu wa karibu waliokuwa kwenye fani hii ya utangazaji lakini kwa juhudi na imani yake juu ya ndoto yake ameweza kuifikia.
Anapenda kufurahi, anapenda utani, anaipenda pia kazi yake na kwake kazi anayoifanya siyo kazi tu ila ni starehe yake.
Ni mtu anayependa kujifunza na anasoma vitu vingi sana.na pia ni muandishi wa simulizi mbalimbali.
Anaamini katika kila changamoto kuna fursa kujifunza ni jambo lisilokuwa na kikomo kwake.