GOZA CHUMA

Goza Msale Chuma lakini nna a.k.a Nyingi ila muhimu ni (“Rais wa Mashabiki”) (“Fundi” ) au “Mshambualiaji mviziaji” Ni mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha Michezo cha KIPENGA TRAXTRA cha East Africa Radio lakini pia ni ni muandishi wa habari na Mtangazaji mbobevu wa masuala ya kijamii, kisiasa na maendeleo.

Vile vile ni Mhariri Msaidizi wa Habari wa kituo cha EATV na East Africa Radio lakini pia ni mtangazaji wa Taarifa ya Habari (New Anchor), East Africa Radio,

Napenda sana kusikiliza muziki na kuongeza marafiki kila siku na lakini napenda sana kufuatilia michezo mbalimbali ikiwemo Soka, Basketball, Boxing na Tennis ila kikubwa ambacho wengi hawakijui ni mwandishi mzuri wa mashairi, muziki wa bongo Fleva, lakini pia ni mshehereshaji (MC) wa shughuli mbalimbali lakini pia ni msanifu mzuri wa sauti (voice artist ) wa matangazo na vipindi maalumu.

Tukutane kwenye Kipenga Xtra kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa sita mpaka saa saba kamili mchana nikiwa na Mashabiki lukuki wa timu mbalimbali duniani.