GEORGE DAVID

Kwa jina ni George David na maarufu kwa jina la kimichezo Central Campister.
Mimi ni mtangazaji na muandaaji wa kipindi cha michezo cha ‘KIPENGA’ East Africa Radio.
Pia nasikika kwenye dondoo mbali mbali za michezo kwenye vipindi mbalimbali pamoja na Saturday Sports kila Jumamosi, saa kumi kamili jioni.
Ni mtu niliyebobea katika masuala ya michezo na nimekua katika tasnia hii kwa miaka kadhaa.
Kupitia ufanisi wa uchambuzi wa michezo ndipo nilipobatizwa jina la ‘CENTRAL CAMPISTER’ ikimaanisha kiungo wa idara ya kati wa Kiitaliano akifananishwa na ubunifi wa Andrea Pirlo kwa namna anavyoweza kutawala dimba katika mechi mbalimbali.
Nje ya utangazaji, Campister ni mjasiliamali anayejihusisha na kilimo na ufugaji.