DJ MACKAY

Jina lake kamili ni Mackay Kilosa lakini wengi wanamjua kwa jina la DJ Mackay “Bulldog” ambaye amekuwa katika tasnia ya utangazaji na DJ kwa miaka zaidi ya kumi na tatu.Alianza kazi yake ya utangazaji na DJ mara tu East Africa Radio ilipoanzishwa na kuendelea na kipaji chake ambacho pia kinaonekana katika kumbi mbali mbali nchini. Akifuata nyayo za kaka zake ambao ni DJ wa muda mrefu wanaokubalika nchini alitamani kufuata nyayo zake na kwa msaada wa kaka zake amefikia alipo sasa.
 
Amewahi kutuzwa zawadi maalum na wasikilizaji kutokana na kuunga kwake mkono sana muziki wa Tanzania hasa 'Afro'. Kwa sasa East Africa Radio ni kati ya maDJ mahiri ambapo amekuwa akiburudisha wasikilizaji katika vipindi mbali mbali vya Redio na Televisheni kama East Africa Drive pamoja na Friday Night Live. Pia amekuwa akifanya kipindi cha Afro Sunday ambacho kinaruka kila Jumapili.