DJ 45 KING

DJ 45 King alianza U-DJ rasmi mwaka 1995 kama DJ wa Club ambapo alipatia umaarufu mkubwa. Na ilipofika mwaka 1999, Aliitwa kuwa mmoja wa waanzilishi wa kituo cha East Africa Radio ambacho anafanya kazi mpaka sasa.

 

Mapenzi yake ya muziki yamemfanya awe DJ anayependelea zaidi kupiga ngoma mpya na zile za zamani zaidi na muda wake wa mapumziko ya kawaida, hupendelea zaidi kujishughulisha na michezo pia kufanya mazoezi ya viungo japo mara tatu kwa wiki.

 

Kwa ngoma kali za Ol Skool na Muziki wa Soul msikilize kwenye Sunday Soul kila Jumapili.