DAVID RWENYAGIRA

Naitwa David Rweikiza Rwenyagira (“Comrade” ) Ni mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha “ EA DRIVE” . Na ni muandishi wa habari na mtangazaji mbobevu katika masuala ya kijamii na maendeleo.
Nimeshinda tuzo ya kuwa mtangazaji bora katika masuala yanahusu utalii wa ndani na uhifadhi, ni balozi mzuri wa masuala ya Afya ya mama na mtoto na uhifadhi wa mazingira.
Vilevile napenda sana kusafiri, muziki na kuongeza marafiki kila siku na msikilizaji wa kipindi changu “Daima ni Mfalme wangu” na namtumikia kwa nguvu, maarifa na ujuzi wangu wote.
Najivunia kuwa msanifu mzuri wa sauti (voice artist ) wa matangazo na vipindi maalumu, ni mshereheshaji ( MC) bora kabisa Tanzania.
“Nakupenda sana na mungu akubariki”